KUTOKANA NA UTUMIAJI WANGU MBOVU WA GOOGLE HAPO MWANZO, LEO HII NAPENDA KUNUKUU;
Hii ni baada ya kugundua ya kwamba hapo mwanzo nilikuwa sifahamu umuhimu wa;
Kwani nilikuwa nikiangalia; picha za ngono, na mambo mengine mengi yasiyopendeza machoni pa Bwana Mungu wetu. Nakuomba nawe ndugu yangu usome na uelewe dhumuni la;
Sheria na Masharti ya Google
Ilibadilishwa mwisho tarehe: 14 Aprili 2014 (
angalia matoleo yaliyohifadhiwa)
Karibu Google!
Asante kwa kutumia bidhaa na huduma zetu (“Huduma”). Huduma zenyewe
zinatolewa na Google Inc. (“Google”), kampuni inayopatikana 1600
Amphitheatre Parkway, Mountain View, CA 94043, United States.
Kwa kutumia Huduma zetu, unakubaliana na masharti haya. Tafadhali yasome kwa makini.
Huduma zetu zinatofautiana, kwa hivyo wakati mwingine masharti ya
ziada au matakwa ya bidhaa (pamoja na masharti ya umri) yanaweza
kutumika. Masharti ya ziada yatapatikana kwenye Huduma husika, na
masharti hayo ya ziada huwa sehemu ya mkataba kati yako nasi kama
unatumia Huduma hizo.
Kutumia Huduma zetu
Lazima ufuate sera zozote zinazotolewa kwako kwenye Huduma zetu.
Usitumie Huduma zetu vibaya. Kwa mfano, usivuruge Huduma zetu au
kujaribu kuzifikia kwa kutumia mbinu nyingine isipokuwa kiolesura na
maagizo tunayotoa. Unaweza kutumia Huduma zetu kama inavyoruhusiwa
kisheria tu, zikiwemo sheria na kanuni husika za kudhibiti uuzaji na
uuzaji tena wa bidhaa kwa nchi za kigeni. Tunaweza kusimamisha au
kusitisha utoaji wa Huduma zetu kwako kama hutafuata masharti au sera
zetu au kama tunachunguza mwenendo mbaya tunaoshuku.
Kutumia Huduma zetu hakukupi umiliki wa hakimiliki zozote katika
Huduma zetu au maudhui unayoyapata. Huwezi kutumia maudhui kutoka kwenye
Huduma zetu bila ruhusa ya mmiliki wake au umeruhusiwa vinginevyo
kisheria kufanya hivyo. Masharti haya hayakupi haki ya kutumia rajamu au
nembo zozote zinazotumiwa katika Huduma zetu. Usiondoe, usifute wala
usibadilishe taarifa zozote za kisheria zinazoonyeshwa ndani ya au
pamoja na Huduma zetu.
Huduma zetu huonyesha maudhui mengine ambayo si ya Google.
Maudhui hayo ni wajibu wa yule anayeyatoa peke yake. Tunaweza kutathmini
maudhui ili kuamua kama ni kinyume cha sheria au yanakiuka sera zetu,
na tunaweza kuondoa au kukataa kuyaonyesha maudhui tunayoamini yanakiuka
sera zetu au sheria. Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba tunatathmini
maudhui kila wakati, kwa hivyo tafadhali usidhani kuwa tunafanya hivyo.
Kuhusiana na matumizi yako ya Huduma, tunaweza kukutumia
matangazo ya arafi za huduma, ujumbe wa usimamizi na maelezo mengine.
Unaweza kuamua kujiondoa kwenye baadhi ya mawasiliano hayo.
Baadhi ya Huduma zetu zinapatikana kwenye vifaa vya mkononi.
Usitumie Huduma kama hizo katika njia ambayo inakutatiza na kukuzuia
kutii sheria za trafiki au za usalama.
Akaunti yako ya Google
Huenda ukahitaji Akaunti ya Google kutumia baadhi ya Huduma zetu.
Unaweza kubuni Akaunti yako ya Google mwenyewe, au unaweza kupewa
Akaunti ya Google na msimamizi, kama vile mwajiri wako au taasisi ya
elimu. Kama unatumia Akaunti ya Google uliyopewa na msimamizi, masharti
tofauti au ya ziada yanaweza kutumika na msimamizi wako anaweza kufikia
au kufunga akaunti yako.
Ili kulinda Akaunti yako ya Google, weka nenosiri lako siri.
Unawajibika kwa shughuli ambayo inafanyika au kupitia Akaunti yako ya
Google. Jaribu kutotumia tena nenosiri lako la Akaunti ya Google kwenye
programu zingine. Ukitambua matumizi yoyote ambayo hayajaidhinishwa ya
nenosiri lako au Akaunti ya Google
fuata maagizo haya.
Ulinzi wa Faragha na Hakimiliki
Sera za faraghaza
Google
huelezea tunavyoshughulikia data yako ya kibinafsi na kulinda faragha
yako unapotumia Huduma zetu. Kwa kutumia Huduma zetu, unakubali kwamba
Google inaweza kutumia data hiyo kulingana na sera zetu za faragha.
Huwa tunajibu taarifa za madai ya ukiukaji wa hakimiliki na
kufunga akaunti za wakiukaji sugu kulingana na utaratibu uliowekwa
katika sheria ya U.S. Digital Millennium Copyright Act.
Tunatoa habari kusaidia wenye hakimilki wadhibiti haki zao za
uvumbuzi mtandaoni. Kama unafikiria kuna mtu anayekiuka hakimiliki zako
na unataka kutujulisha, unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya
kuwasilisha taarifa na sera ya Google
kuhusu kujibu ilani kwenye Kituo chetu cha Msaada.
Maudhui yako katika Huduma zetu
Baadhi ya Huduma zetu zinakuruhusu upakiE, uwasilishe, utume au
upokee maudhui. Unabakia na umiliki wa haki zozote za uvumbuzi ambazo
unazo katika maudhui hayo. Kwa ufupi, kilicho chako kinabaki chako.
Unapopakia, wasilisha, hifadhi, kutuma au kupokea maudhui kwenye
au kupitia Huduma zetu, unaipa Google (na wale ambao tunafanya kazi nao)
leseni ya duniani kote ya kutumia, kupangisha, kuhifadhi, kuzalisha
upya, kurekebisha, kuunda miigo ya kazi (kama ile inayotokana na
kutafsiri, marekebisho au mabadiliko mengine tunayoyafanya ili maudhui
yako yafanye kazi vyema na Huduma zetu), kuwasiliana, kuchapisha,
kutekeleza hadharani, kuonyesha hadharani na kusambaza maudhui kama
hayo. Haki unazotoa katika leseni hii ni ya nia ya uendeshaji, ukuzaji,
na kuboresha Huduma zetu, na kukuza mpya. Leseni hii inaendelea hata
kama utawacha kutumia Huduma zetu (kwa mfano, kwa orodha ya biashara
ulyioongeza kwenye Ramani za Google). Baadhi ya Huduma zinaweza kupa
njia za kufikia na kuondoa maudhui ambayo yametolewa kwa Huduma hiyo.
Pia, katika baadhi ya Huduma zetu, kuna masharti au mipangilio inayo
punguza eneo la utumiaji wetu wa maudhui yaliowasilishwa katika huduma
hizo. Hakikisha una haki zinazohitajika kutupa leseni kwa maudhui yoyote
ambayo unawasilisha kwa Huduma zetu.
Mifumo yetu ya kiotomatiki huchanganua maudhui yako (ikiwa ni
pamoja na barua pepe) ili kukupa kibinafsi vipengele husika vya bidhaa,
kama vile matokeo ya utafutaji yaliobinafsishwa, utangazaji ulio
binafsishwa, na ugunduaji barua taka na programu hasidi. Uchambuzi huu
hutokea wakati maudhui yanatumwa, kupokewa, na wakati yanahifadhiwa.
Ikiwa una Akaunti ya Google, tunaweza kuonyesha jina lako la
Wasifu, picha ya Wasifu, na vitendo unavyovichukua kwenye Google au
kwenye programu zingine zilizounganishwa kwenye Akaunti yako ya Google
(kama vile +1, ukaguzi unaouandika na maoni unayoyachapisha) katika
Huduma zetu, ikiwa ni pamoja na kuonyesha katika matangazo na miktadha
mingine ya kibiashara. Tutaheshimu chaguo utakazozifanya ili kuzuia
kushiriki au mipangilio ya mwonekano katika Akaunti yako ya Google. Kwa
mfano, unaweza kuchagua mipangilio yako ili jina na picha yako
zisionekane katika tangazo.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia na
kuhifadhi maudhui katika sera ya faragha au masharti ya ziada ya Huduma
mahususi. Ukitoa maoni au mapendekezo kuhusu Huduma zetu, tunaweza
kutumia maoni na mapendekezo yako bila kuwajibika kwako.
Kuhusu Programu katika Huduma zetu
Wakati Huduma inahitaji au inajumuisha programu inayoweza kupakuliwa,
programu hii inaweza kujisasisha kiotomatiki kwenye kifaa chako mara
toleo jipya au kipengee kipya kinapopatikana. Baadhi ya Huduma zinaweza
kukuruhusu urekebishe mipangilio yako ya kujisasisha.
Google inakupa leseni ya kibinafsi, duniani kote, bila ada,
isiyoweza kuhamishwa kwa mwingine na isiyowaondoa wengine, ya kutumia
programu iliyotolewa kwako na Google kama sehemu ya Huduma. Leseni hii
lengo lake la pekee ni kukuwezesha kutumia na kufurahia faida ya Huduma
kama zinavyotolewa na Google, kwa jinsi inayoruhusiwa na masharti haya.
Huruhusiwi kunakili, kubadilisha, kusambaza, kuuza au kukodisha sehemu
yoyote ya Huduma zetu au programu zilizojumuishwa, wala huruhusiwi
kufanya uhandisi wa kinyume au kujaribu kudondoa msimbo asili wa
programu hiyo, isipokuwa sheria iwe inazuia vikwazo hivyo au una ruhusa
yetu kimaandishi.
Programu huria ni muhimu kwetu. Baadhi ya programu zinazotumika
katika Huduma zetu zinaweza kutolewa chini ya leseni ya programu huria
ambayo tutatoa kwako. Kunaweza kuwa na vipengele katika leseni ya
programu huria ambavyo vinabatilisha baadhi ya masharti haya.
Kubadilisha na Kukatisha Huduma zetu.
Tunabadilisha na kuboresha Huduma zetu kila wakati. Tunaweza kuongeza
au kuondoa utendakazi au vipengee, na tunaweza kusimamisha au kusitisha
Huduma kabisa.
Unaweza kuacha kutumia Huduma zetu wakati wowote, ingawa
tutasikitika kukupoteza. Google inaweza kuacha kukupa Huduma, inaweza
pia kuongeza au kuweka mipaka mipya kwa huduma zetu wakati wowote.
Tunaamini kuwa unamiliki data yako na kuhifadhi ufikiaji wako kwa
data hiyo ni muhimu. Tukiondoa Huduma, inapowezekana, tutakupa ilani ya
muda ufaao na nafasi ya kuondoa maelezo kwenye Huduma hiyo.
Hakikisho na Kanusho Zetu
Tunatoa Huduma zetu kwa kutumia kiwango cha ujuzi na uangalifu wa
kibiashara unaofaa na tunatumaini utafurahia kuzitumia. Lakini kuna
mambo fulani ambayo hatuahidi kuhusu Huduma zetu.
ISIPOKUWA KAMA ILIVYOTAJWA WAZIWAZI KATIKA MASHARTI HAYA AU
MASHARTI YA ZIADA, GOOGLE, WATOA HUDUMA AU WASAMBAZAJI WAKE HAWATOI
AHADI YOYOTE MAHUSUSI KUHUSU HUDUMA. KWA MFANO, HATUTOI AHADI ZOZOTE
KUHUSU MAUDHUI KATIKA HUDUMA, UTENDAKAZI MAHUSUSI WA HUDUMA, AU UTHABITI
WAKE, UPATIKANAJI, AU UWEZO WA KUTIMIZA MAHITAJI YAKO. TUNATOA HUDUMA
“KAMA ILIVYO”
BAADHI YA MAENEO YA UTAWALA HUTOA HAKIKISHO FULANI, KAMA VILE
HAKIKISHO LISILOTAJWA LA KUFAA KWA MAUZO, KUFAA KWA LENGO FULANI NA
KUTOUKIUKA. KADRI INAVYORUHUSIWA NA SHERIA, TUNAONDOA HAKIKISHO LOLOTE.
Dhima ya Huduma zetu
WAKATI IMERUHUSIWA NA SHERIA, GOOGLE, NA WATOA HUDUMA NA WASAMBAZAJI
WAKE, HAWATAWAJIBIKA KWA FAIDA ILIYOPOTEA, MAPATO, AU DATA, HASARA YA
FEDHA AU FIDIA MAALUM, ISIYO YA MOJA KWA MOJA, YA KUAMBATANA, AU YA
KIPEKEE.
KADRI INAVYORUHUSIWA NA SHERIA, JUMLA YA DHIMA YA GOOGLE, NA
WATOA HUDUMA NA WASAMBAZAJI WAKE, KWA MADAI YOYOTE CHINI YA MASHARTI
HAYA, PAMOJA NA HAKIKISHO ZILIZODOKEZWA, ITAKOMEA IDADI YA PESA
ULIYOTULIPA KUTUMIA HUDUMA (AU, TUKICHAGUA, KUKUPA HUDUMA TENA).
KATIKA HALI ZOTE, GOOGLE NA WATOA HUDUMA NA WASAMBAZAJI WAKE,
HAWATAWAJIBIKA KWA HASARA AU UHARIBIFU AMBAO HAUWEZI KUTARAJIWA KWA
KAWAIDA.
Matumizi ya kibiashara ya Huduma zetu
Kama unatumia Huduma zetu kwa niaba ya biashara, biashara hiyo
inayakubali masharti haya. Itaichukulia Google kuwa bila hatia na
itaifidia pamoja na washirika wake, maafisa, mawakala, na wafanyakazi
kutokana na madai yoyote, mashtaka au kesi kutokana na au kuhusiana na
matumizi ya Huduma au ukiukaji wa masharti haya, ikiwa ni pamoja na
dhima au gharama yoyote kutokana na madai, hasara, uharibifu, mashtaka,
hukumu, gharama za mashtaka na ada za wakili.
Kuhusu Masharti haya
Tunaweza kubadilisha masharti haya au masharti ya ziada yanayotumika
kwa Huduma, kwa mfano, kuonyesha mabadiliko katika sheria au mabadiliko
katika huduma zetu. Inafaa uangalie masharti haya mara kwa mara.
Tutaweka taarifa za marekebisho ya masharti haya kwenye ukurasa huu.
Tutaweka taarifa ya masharti ya ziada yaliyorekebishwa katika Huduma
husika. Mabadiliko hayatatekelezwa kwa wakati uliopita na yataanza
kufanya kazi baada ya angalau siku kumi na nne baada ya kuchapishwa.
Lakini, mabadiliko yanayoshughulikia utendakazi mpya wa Huduma au
mabadiliko yaliyofanywa kwa sababu za kisheria yatatumika mara moja.
Kama hukubaliani na masharti yaliyobadilishwa ya Huduma fulani, unfaa
uache kutumia Huduma hiyo.
Kama kuna ukinzani kati ya masharti haya na masharti ya ziada, masharti ya ziada yatadhibiti ukinzani huo.
Masharti haya yadhibiti uhusiano kati yako na Google. Hayaleti haki zozote kufaidi mhusika mwingine.
Kama hutii masharti haya, na hatuchukui hatua mara moja, hii
haimaanishi ya kwamba tunasalimisha haki zozote ambazo tunazo (kama vile
kuchukua hatua baadaye).
Ikitokea kwamba sharti fulani haliwezikutekelezwa, hili halitaathiri masharti mengine yoyote.
Sheria za California, U.S.A, isipokuwa sheria za mgongano wa
sheria za California, zitatumika kwa mizozo yoyote kutokana au kuhusiana
na masharti haya au Huduma. Mashtaka yote yanayotokana na au
yanayohusiana na masharti haya au Huduma, yatapelekwa katika mahakama za
nchi au jimbo la Santa Clara, California, USA, na wewe na Google
mnakubali kuwa chini ya mamlaka ya sheria katika mahakama hizo.