Ijumaa, 15 Mei 2015

JIBU NA ELIMU NILIYOMPA RAFIKI YANGU KIPENZI AMBAE ALIJALIBU KUTAKA KUNISHAWISHI ILI NICHUKIE DINI NYINGINE!



Basi nawe kama una ushauri, basi jitoe ili tufundishane.
Uumbe moyo safi ndani yangu, Ee Mungu, Na kuweka ndani yangu roho mpya, iliyo imara.


Kabla sijakujibu, ebu nikwambie; "nimefurahi sana ulivyo jibu hivyo" kwani Mungu anamakusudi yake. Unajua sisi bado atujajua kwamba Dini ni nini?, Dini ni jina tu kama majina mengine, ila Wokovu ni kitendo cha kukubali kwamba; "Umekubali kumkataa shetani na dhambi zake zote, na kukubali kumpokea Mungu kuwa bwana na Mkombozi wa maisha yako".

Basi sasa, sisi kama wote ni Binadamu, hatupaswi kugombana wala kukashifiana kwa sababu ya Dini!. Sasa nachokuomba ndugu yangu unielewe kwamba; "Dini zote tuna amini kwamba tunaishi kwa sababu ya Mungu", basi sasa ngoja nikutume ili uende ukawaambie na wenzako kwamba; "Hapo mwanzo Mungu aliumba Mbingu na Dunia. Dunia ilikuwa bila umbo, na ukiwa, na giza lilikuwa juu ya uso wa kilindi cha maji, na nguvu za utendaji za Mungu zilikuwa zikienda huku na huku juu ya uso wa maji", basi Mungu akaendelea kufanya mambo mengi sana hadi sisi kufikia hapa tulipo. Ila kama ukifuatilia sana mbele utakuja kuana kwamba, Mungu akamtuma mwanae ambae anaitwa Bwana na Mkombozi wa maisha yetu, Kristo Yesu, ambaye alikuwapo hata katika dini zingine akitambulika kwa jina la; "Bwana na Mkombozi wa maisha yetu 'Isa Ibn Maryam', ambaye ukifuatilia historia yake utagundua ya kwamba kila sehemu alikuwa na jina lake.akaendelea.

 Na ubarikiwe sana ndugu yangu. Kwani nimetambua kwamba Mungu anakupenda, hadi ikafikia hatua ya wewe kuniuliza swali kama ilo. Amini kwamba Mungu yupo na anatenda. Amina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni