Ijumaa, 15 Mei 2015

FUNDISHWA, FUNDISHA, FUNDISHO LENYE AFYA


Hawa ndio Mungu aliwachagua ili waje wanifundishe juu ya neno Takatifu la Mwenyezi Mungu kwa kupitia Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai milele na milele. Pia na nyie ndugu zangu wote kokote mlipo basi pokeeni shukrani zangu. Amina.
Mbarikiwe sana Baba zangu ambao mmenitoa kutoka katika Dunia iliyokuwa bila umbo, na ukiwa, na giza lilikuwa juu ya uso wa kilindi cha maji, na nguvu za utendaji za Mungu zilikuwa zikienda huku na huku juu ya uso wa maji. Ila Mungu mwenyewe akasema; "Kuwe na nuru." kukawa na nuru. Kisha Mungu akaona ya kuwa nuru ilikuwa nzuri. Mungu akatenganisha nuru na giza. Na sasa nipo hivi nilivyo.
Kwahiyo napenda kuwa ambia ndugu zangu kwamba; "Mungu yupo na anatenda kazi zake kila siku, anasubiri, mtu amuite ili aanze kutenda kazi. Basi sasa, Kama wewe ni, wa, Dini yeyote hile Ninacho kuomba nennda unakokujua na kisha umrudie Mungu wako.
Fadhili zisizostahiliwa za Bwana Yesu Kristo na ziwe pamoja na watakatifu.
Amina.

Maoni 1 :

  1. Mungu asema: "Na wana wako wote watakuwa watu waliofundishwa na Yehova, na amani ya wana wako itakuwa nyingi. Amina.

    JibuFuta