Kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo lazima yatendeke upesi. Naye alimtuma malaika wake na kupitia yeye akautoa kwa njia ya ishara kwa mtumwa Yohana, aliyetoa ushahidi kuhusu neno ambalo Mungu alitoa na kuhusu ushahidi ambao Yesu Kristo alitoa, naam, kuhusu mambo yote aliyoyaona. Mwenye furaha ni yeye anayesoma kwa sauti na wale wanaosikia maneno ya unabii huu, na wanaoshika mambo yaliyoandikwa humo, kwa maana wakati uliowekwa uko karibu.
Yohana kwa makutaniko saba yaliyo katika wilaya ya Asia:
Na muwe na fadhili zisizostahiliwa na amani kutoka kwa "Yule aliyeko na aliyekuwako na anayekuja, na kutoka kwa zile roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha ufalme, na kutoka kwa yesu Kristo, "Shahidi Mwaminifu," Mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, na "Mtawala wa wafalme wa dunia."
Kwake yeye anayetupenda na aliyetufungua kutoka katika dhambi zetu kupitia damu yake mwenyewe- naye alitufanya tuwe ufalme, makuhani kwa Mungu na Baba yake- ndiyo, kwake yeye na kuwe na utukufu na nguvu milele. Amina.
Tenzi za Rohoni namba 34. "Njoni Wenye Dhambi"
Njoni! Njoni! Wenye dhambi,
Njoni, msikawie;
Yesu awangojea ndiye awapendaye;
Ajuaye awezaye
kuwaponya ni yeye.
Ewe muhitaji uje;
Anakukaribisha,
Imani, kweli, na toba,
Neema ya kutosha,
Jua sana, kwake Bwana
Bure utapata.
Njoni, mliolemewa
Na dhambi ya Adamu;
Mkingoja kujiponya
Mtapotea mumu;
Si wa haki, ni wakosa
Waoshwao kwa damu.
Ikamtokea dhiki,
Mle Gethisemani;
Kisha alipoangikwa
Akalia mtini;
"Imekwisha" alitosha
Dhabihu ya thamani.
Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea huko;
Basi mtumai yeye;
Kamwe mwingine hako
Yesu pweke, Yesu pweke,
Ndiye Mwokozi wako.
Wamsifu-sifu sana
Mbinguni malaika;
Wachanganya nyimbo zao
Na waliookoka:
Aleluya wataimba
Waliooshwa taka.
"Yeye anayetoa ushahidi juu ya mambo haya asema, "Ndiyo; mimi ninakuja upesi'."
"Amina! Njoo, Bwana Yesu"
Fadhili zisizostahiliwa za Bwana Yesu Kristo na ziwe pamoja na watakatifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni