Sera ya Maudhui ya Blogger
Blogger ni huduma ya bila malipo ya kuwasiliana, kujieleza na uhuru
wa mazungumzo. Tunaamini kuwa Blogger huongeza upatikanaji wa habari,
huhimiza mijadala bora, na hurahisisha miunganisho mipya kati ya watu.
Ni imani yetu kwamba kudhibiti maudhui haya ni kinyume na huduma
inayozingatia uhuru wa kujieleza.
Hata hivyo, ili kuendeleza maadili haya, tunahitaji kukabiliana na
ukiukaji ambao unatishia uwezo wetu wa kutoa huduma hii na uhuru wa
kujieleza unaohimizwa. Kwa hivyo, kuna mipaka kuhusu aina ya maudhui
ambayo yanaweza kutumika kwenye Blogger. Mipaka ambayo tumeweka ni ile
ambayo inaafikiana na mahitaji ya kisheria na kuboresha huduma kwa
jumla.
Kama utaona blogu ambayo unaamini kuwa inakiuka sera zetu, tafadhali
tueleze kwa kutumia kiungo cha 'Ripoti Matumizi Mabaya' kinachopatikana
sehemu ya juu ya kila blogu chini ya menyu kunjuzi ya 'Zaidi'. Kama
mmiliki wa blogu ameficha kiungo hiki, bado unaweza
kuripoti matumizi mabaya katika Kituo cha Msaada cha Blogger.
Mipaka ya Maudhui
Sera zetu za maudhui zina jukumu muhimu katika kuwadumishia matumizi
mazuri, nyinyi watumiaji. Tafadhali heshimu maelekezo haya. Mara kwa
mara, tunaweza kubadilisha sera zetu za maudhui kwa hivyo tafadhali
rejelea hapa. Pia, tafadhali kumbuka kuwa wakati wa kutumia sera zilizo
hapo chini, tunaweza kutofuata kanuni kwa msingi wa kisanii, kielimu,
filamu ionyeshayo hali halisi, au kisayansi au ambapo kuna manufaa
mengine makubwa kwa umma kutokana na kutoyachukulia maudhui hatua.
Maudhui ya Watu Wazima:
Tunaruhusu maudhui ya watu wazima kwenye Blogger, ikiwa ni pamoja na
picha au video zenye watu walio uchi au shughuli za kufanya mapenzi.
Lakini, alamisha blogu yako kama ya 'watu wazima' katika mipangilio ya
Blogger yako. Tunaweza kualamisha blogu zilizo na maudhui ya watu wazima
ambazo wenyewe hawajazialamisha. Blogu zote ambazo zimealamishwa
'maudhui ya watu wazima' zitawekwa chini ya kitengo cha 'maudhui ya watu
wazima'. Ikiwa blogu yako ina onyo la kitengo, tafadhali usijaribu
kukiondoa au kuzima kitengo hicho - ni cha kulinda kila mtu.
Sera yetu ya maudhui ya watu wazima inaweza kubatilishwa:
- Usitumie
Blogger kuchuma pesa kutoka kwa maudhui ya watu wazima. Kwa mfano,
usiunde blogu zilizo na matangazo au viungo vya tovuti za biashara ya
filamu za ngono.
- Haturuhusu maudhui ya picha, video au maandishi yanayoashiria ubakaji, kufanya ngono na jamaa, wanyama au maiti.
- Usichapishe au kusambaza picha za kibinafsi za uchi au picha za kingono au video zako, tafadhali ziripoti kwetu hapa.
Usalama wa watoto: Tuna sera isiyoruhusu kabisa maudhui yanayowanyanyasa watoto. Baadhi ya mifano ya hii ni pamoja na:
- Ponografia ya watoto:Tutafuta
akaunti za mtumiaji yeyote tutakayepata akichapisha au kusambaza
ponografia ya watoto. Pia tutamripoti mtumiaji huyo kwa watekelezaji wa
sheria.
- Ashiki ya watoto: Haturuhusu maudhui
yanayohimiza au kukweza mvutio wa kingono kwa watoto. Kwa mfano,
usifungue blogu zilizo na ghala za picha za watoto ambapo mkusanyiko wa
picha au maandishi yanayoambatana na picha ni ya kulenga tabia za
kingono.
Matamshi ya Chuki: Huduma zetu ni jukwaa la kutoa
maoni bila ya vikwazo. Lakini haturuhusu maudhui yanayoendeleza chuki au
vurugu dhidi ya makundi kwa msingi wa rangi, ukabila, dini, ulemavu,
jinsia, umri, hali ya kuwahi kuwa mwanajeshi, au mwelekeo wa
kingono/jinsia au ambayo misingi yake ni kueneza chuki kwa misingi ya
sifa hizi. Hili linaweza kuwa suala nyeti, lakini ikiwa lengo kuu ni
kushambulia kundi lililolindwa, basi maudhui yamepita mipaka.
Maudhui Ghafi: Usichapishe maudhui ili kutisha au
kuudhi. Kwa mfano, mikusanyiko ya picha za karibu za majeraha ya risasi
au matukio ya ajali bila maudhui au maelezo ya ziada yatakeuka sera hii.
Vurugu: Usiwatishe watu wengine kwenye blogu yako.
Kwa mfano, usichapishe vitisho vya mauaji dhidi ya mtu au kundi lingine
la watu na usichapishe maudhui yanayowahimiza wasomaji wako kuchukua
hatua ya vurugu dhidi ya mtu mwingine au kundi lingine la watu.
Unyanyasaji: Usinyanyase au kuwachokoza wengine.
Yoyote anayetumia Blogger kunyanyasa au kuchokoza anaweza maudhui
yanayochukiza kuondolewa na anaweza kupigwa marufuku kabisa kwenye
tovuti. Unyanyasaji wa mtandaoni pia sio halali katika maeneo mengi na
unaweza kuwa na athari mbaya sana nje ya mtandao.
Hakimiliki: Ni sera yetu kujibu arifa wazi za madai
ya ukiukaji wa hakimiliki. Maelezo zaidi kuhusu taratibu zetu za
hakimiliki yanaweza kupatikana
hapa.
Pia, tafadhali usitoe viungo kwa tovuti ambazo wasomaji wako wanaweza
kutekeleza upakuaji usioruhusiwa wa maudhui ya watu wengine.
Maelezo ya kibinafsi na ya faragha: Si sawa
kuchapisha maelezo ya kibinafsi na ya faragha ya mtu mwingine. Kwa
mfano, usichapishe nambari za kadi ya mkopo, nambari za Usalama wa
Jamii, nambari za simu zisizoorodheshwa, na nambari za leseni ya dereva
za mtu mwingine. Pia, tafadhali kumbuka kuwa mara nyingi, maelezo ambayo
tayari yanapatikana pahali pengine kwenye mtandao au katika rekodi za
umma hayachukuliwi kuwa ya kibinafsi au ya faragha chini ya sera zetu.
Kuiga wengine: Tafadhali usiwapotoshe au
kuwachanganya wasomaji kwa kujifanya kuwa mtu mwingine au kujifanya
kuwasilisha shirika. Hatusemi huwezi kuchapisha mwigo wa kubeza au
tashtiti - epuka tu maudhui yanayoweza kupotosha wasomaji kuhusu
utambulisho wako halisi.
Shughuli haramu: Usitumie Blogger kujihusisha katika
shughuli haramu au kuundeleza shughuli hatari na haramu. Kwa mfano,
usiandike blogu inayowahimiza watu kuendesha gari wakiwa walevi.
Tafadhali pia usitumie Blogger kuuza au kutangaza mihadarati.
Vinginevyo, tunaweza kufuta maudhui yako. Pia, katika hali mbaya kama
zinazohusisha unyanyasaji wa watoto, tunaweza kukushtaki kwa mamlaka
husika.
Bidhaa na Huduma Zilizodhibitiwa: Usitumie Blogger
kuuza au kurahisisha uuzaji wa bidhaa na huduma zilizodhibitiwa, kwa
mfano pombe, karata, dawa na nyongeza ambazo hazijaidhinishwa, tumbaku,
fataki, silaha au vifaa vya afya/matibabu.
Taka: Taka ni za aina mbalimbali katika Blogger,
zote zinaweza kusababisha ufutaji wa akaunti au blogu yako. Baadhi ya
mifano ni pamoja na kufungua blogu zilizoundwa kuendesha trafiki kwenye
tovuti yako au kuisogeza juu katika orodha ya utafutaji, kuchapisha
maoni kwenye blogu za watu wengine ili tu kuendeleza tovuti au bidhaa
yako, na kuchapisha maudhui kutoka nyenzo nyingine kwa madhumuni msingi
ya kuzalisha mapato au manufaa mengine ya kibinafsi.
}Programu hasidi na virusi: Usiunde blogu
zinazosambaza virusi, kusababisha madirisha-ibukizi, kujaribu
kusakinisha programu bila idhini ya msomaji au vinginevyo kuwaathiri
wasomaji na msimbo hasidi. Haya hayaruhusiwi kabisa kwenye Blogger.
Utekelezaji wa Sera ya Maudhui ya Blogger
Tafadhali tupe ripoti ya tuhuma za ukiukaji wa sera kwa kutumia
kiungo cha 'Ripoti Matumizi Mabaya ' kinachopatikana sehemu ya juu ya
kila blogu chini ya menyu kunjuzi ya ' Zaidi' au kwa kubofya
hapa.
Timu yetu hukagua ripoti za wanaotumia huduma kuhusu ukiukaji wa
sera. Kama blogu haikiuki sera zetu, hatutachukua hatua yoyote dhidi ya
blogu hiyo au mmiliki wa blogu. Kama tutatambua kuwa blogu inakiuka sera
zetu za maudhui, tutachukua mojawapo wa hatua zifuatazo, kulingana na
kiwango cha ukiukaji:
- Weka blogu nyuma ya skrini ya ' maudhui ya watu wazima & # 39;
- Weka blogu nyuma ya skrini ambapo ni mwandishi wa blogu pekee ndiye anayeweza kufikia maudhui
- Futa maudhui mabaya, chapisho la blogu au blogu
- Zima uwezo wa mwandishi wa kufikia akaunti yake ya Blogger
- Zima uwezo wa mwandishi wa kufikia akaunti yake ya Google
- Ripoti mtumiaji kwa watekelezaji wa sheria
Tunaweza pia kuchukua hatua yoyote iliyo hapo juu iwapo tutagundua
kuwa mtumiaji ameunda blogu nyingi zinazojihusisha na tabia ya matusi.
Ikiwa una blogu iliyofungwa, usiunde blogu badala inayojihusisha na
shughuli kama hiyo.